Mwandishi Wetu, Dodoma      |
Serikali imesema itaendelea kusimamia na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa shule na vyuo vinavyomilikiwa na taasisi binafsi nchini.
Pia itaendelea kufanya hivyo kwa shule za serikali ili kuhakikisha elimu inayotolewa ni bora na inakidhi vigezo.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la papo hapo aliloulizwa na Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu (CCM), aliyetaka kujua ni hatua gani zinachukuliwa na serikali katika kuhakikisha taasisi binafsi zinatoa elimu bora.
“Serikali imetoa fursa kwenye taasisi binafsi kuwekeza katika sekta ya elimu lakini pia inaratibu ili kujiridhisha elimu, nidhamu na malezi yanakuwa katika ubora.
Aidha, amesema Serikali itaendelea kusimamia maadili na nidhamu kwa shule binafsi ili ubora wa elimu uzidi kuongezeka.