PARIS, UFARANSA
NYOTA wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa, Serge Aurier, amehukumiwa kwenda jela miezi mwili kwa kosa la kumgonga afisa wa polisi Mei mwaka huu.
Beki huyo wa timu ya taifa ya Ivory Coast, inadaiwa kwamba alimgonga polisi nje ya kumbi ya starehe na inadaiwa kwamba mchezaji huyo alikuwa amekunywa pombe na kusababisha kutokea kwa tukio hilo.
Hata hivyo kutokana na kosa hilo, inadaiwa kwamba mchezaji huyo hawezi kwenda jela lakini anatakiwa kulipa faini ya dola 674.
Aurier mwenye umri wa miaka 23, alifikishwa mahakamani jana na kusomewa shitaka lake. Mwanasheria wa mchezaji huyo amedai kwamba kwa sasa wanasubiri rufaa yao.
Mchezaji huyo kwa sasa bado yupo huru huku akisubiri rufaa yake na anaweza kuwa uwanjani katika mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya katika hatua ya makundi.
Juni mwaka huu baada ya tukio hilo, mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Lens na Toulouse, aliiambia televisheni ya Ufaransa kwamba, ilikuwa ni vurugu kati yake ya maafisa wa polisi.
“Ilikuwa ni vurugu kubwa kati yangu na maafisa wa polisi, ilifikia hatua walinitukana na walinitoa kwenye gari yangu kwa nguvu na kunifanyia ukatili kwa na waliweza kuniumiza mdomo.
“Lakini mbaya zaidi nilishangaa kwamba afisa wa polisi alisema nilikuwa nimemuumiza katika kifua chake wakati ukweli ni kwamba sikufanya lolote zaidi ya wao kunishambulia usoni, siwezi kuficha chochote ambacho kilitokea siku hiyo na wapo mashahidi watano au sita ambao wanaweza kuweka sawa jambo hilo.