25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

Liewig atamba kuendeleza vipigo

liewigNa MASYENENE DAMIAN-SHINYANGA

KOCHA mkuu wa timu ya Stand United, Patrick Liewig, ametamba kuwa wataendeleza vipigo katika Ligi Kuu Tanzania Bara na kudai kwamba matokeo ya ushindi kwa kikosi chake hayajalishi wanakutana na timu kubwa au ndogo kwenye ligi hiyo.

Kikosi cha kocha huyo raia wa Ufaransa, juzi kilitibua rekodi ya Yanga ya kutofungwa tangu kuanza kwa Ligi Kuu msimu huu baada ya kuwalaza kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Liewig alisema wachezaji waliingia uwanjani na kucheza wakiwa wametulia na kujituma huku wakifuata mbinu na maelekezo aliyowapa.

“Utulivu wao ulisaidia kujipanga vyema uwanjani hivyo kuwafanya Yanga washindwe kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, juhudi hizi ni lazima ziendelee,” alisema.

Matokeo ya ushindi dhidi ya Yanga yamewapa jeuri Stand ya kutamba kuendeleza kasi hiyo ligi kuu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kumaliza katika nafasi nne za juu.

Kwa sasa Stand inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 12 nyuma ya vinara Simba wanaoongoza kwa kujikusanyia pointi 16 zote zikiwa zimecheza michezo sita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,682FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles