25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serengeti Boys kwenda Korea Kusini leo

KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’
KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’

Na MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, kinatarajia kuondoka leo saa 10:30 jioni kuelekea nchini Korea Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana yatakayoanza kesho nchini humo.

Msafara huo wa wachezaji 16 na viongozi sita, utaongozwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi pamoja na Mshauri wa Ufundi na Maendeleo kwa soka la vijana, Kim Poulsen.

Kwa upande wa benchi ya ufundi litaongozwa na kocha mkuu, Bakari Shime, Muharami Mohamed, anayewanoa makocha, daktari Shecky Mngazija na Meneja Edward Venance.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo, Serengeti Boys itacheza michezo mitatu kusaka tiketi ya kuingia fainali.

“Timu itaondoka saa 10:30 jioni kwa ndege ya Shirika la Emirates kupitia Dubai ambako wataunganisha ndege nyingine kuelekea Korea Kusini,” alisema.

TFF imepanga mikakati ya kuiingiza Serengeti Boys katika programu ya timu ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’, ili kuiandaa kufanya vyema kwenye michuano ya Fainali za Vijana Afrika zikazofanyika hapa nchini mwaka 2019.

Serengeti Boys ilishindwa kufuzu kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika nchini Madagascar mwakani baada ya kutolewa na Congo Brazzaville katika raundi ya pili ya michuano hiyo.

Wakati huo huo, timu ya soka ya Taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’, iliondoka jana kuelekea mjini Yaounde, Cameroon kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaopigwa nchini humo.

Kikosi cha Twiga Stars kinachonolewa na kocha Sebastian Nkoma, kiliondoka na nyota 17 na viongozi sita kwa ndege ya Shirika la Kenya (KQ) kupitia jijini Nairobi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles