27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi FBI aingia matatani

Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), Jamey Comey
Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), Jamey Comey

NA JUSTIN DAMIAN, ALIYOKO MAREKANI

BAADA ya kumsafisha mgombea wa urais wa Chama cha Democrat,Hillary Clinton kutokana na kashfa ya barua pepe, Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), Jamey Comey ameingia matatani.

Hatua  isiyo ya kawaida ya shirika hilo kushughulikia suala nyeti kama la Clinton ndani ya siku tisa, inaelezewa kuwa itakuwa na madhara ya makubwa kwa FBI na mkurugenzi huyo ambaye mkataba wake wa miaka kumi unaishia 2023.

Seneta wa California, Dianne Feinstein ambaye ni mjumbe maarufu wa kamati ya mahakama inayoisimamia FBI alisema, uamuzi wa mkurugenzi huyo kumsafisha Clinton umezua utata mkubwa.

“Namna ambavyo suala hili limeshughulikiwa limetengeneza hisia mbaya ya jinsi ambavyo FBI imelifanyia kazi. Naamini Idara ya Haki inahitaji kutizama taratibu zilizotumika ili kuepuka vitendo vya aina hii vinavyoweza kujitokeza kwenye chaguzi zijazo,” alisema

Wito wa uchunguzi mpya wa suala hilo, umetolewa na Seneta wa Maryland, Elijah Cummings ambaye ni mjumbe wa kamakati ya masuala ya serikali kutoka Democrat na Seneta wa Michigan, John Conyers ambaye ni ofisa wa juu katika Kamati ya Sheria ya Seneti kutoka Chama cha Republican. Maseneta wengi wanataka uchunguzi kufanyika na kubaini kama kweli FBI walivujisha siri kwenye kambi ya Trump siku za mwisho kabla ya uchaguzi

“Siku za mbeleni, tutakuwa na maswali mengi zaidi ya namna FBI ilivyofanya uchunguzi juu ya jambo hili,” alieleza.

Ni mara chache kwa vyama  vikubwa viwili vya Republican na Democrat kukubaliana juu ya jambo fulani, lakini katika hali isiyo ya kawaida suala la kutaka taarifa zaidi kuhusuiana na suala hilo kutoka kwa mkurugenzi wa FBI limeweza kuwaunganisha.

Seneta wa Iowa,Charles Grassley ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Seneti ambaye pia amekuwa akikosoa utendaji wa FBI, alisema suala la kumsafisha Clinton kama taarifa iliongeza utata.

“Kwa miezi sasa nimekuwa nikiwataka FBI kutoa taarifa zaidi kuhusiana na namna walivyolishughulikia suala la Clinto. Wamarekani wana haki ya kujua kama FBI walikuwa wanachunguza kama Clintomn wakati akiwa Maziri wa Mambo ya Nje na msaidizi wake walivunja sheria,” alisema

Wakati Congress wanaweza kulishinikiza shirika hilo kutoa taarifa zaidi kupitia Mkaguzi Mkuu wa Idara ya Haki, wachambuzi wa mambo wanasema mkurugenzi huyo na FBI kwa ujumla wanaweza wkuwa katika wakati mgumu baada ya Rais mpya kuingia Ikulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles