33.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

SCOTT EDWARD ADKINS ‘BOYKA’ MKALI WA MAPIGANO

Kama mfuatiliaji wa filamu za mapigano, majina ya filamu hizi si mageni kwako ‘Hard Tarfet 2’, ‘Close Range’, ‘Wolf Warrios’, ‘Jarhead’, ‘El Gringo’, ‘Ninja: Shadow of a Tear’, ‘Eliminators’, ‘Zero Tolerance’, ‘Legendary’, ‘Boyka Undisputed’, ‘Doctor Strange’, ‘Undistibuted 2’, ‘Undistibuted III, Redemption’.

Majina hayo ni ya filamu ambazo mtaalamu wa filamu za mapigano, Scott Edward Adkins ambaye wengi wanamwita (Boyka), amezicheza kwa ustadi mkubwa na wa kuvutia mno.

Mkali huyu tunayeanza naye kwenye safu hii, amezaliwa Juni 17, mwaka 1976 huko Sutton nchini Uingereza.

Filamu za Scott Adkins zinaonyeshwa zaidi kwenye magari ya abiria na familia kwa kuwa zimezingatia maadili ya kuheshimu uhuru wa watoto wadogo kwa kutokuweka vipengele visivyotakiwa kuonwa na watoto walio chini ya miaka 18.

Alianza kupenda michezo ya mapigano alipokuwa na miaka 10 ambapo baba yake mzazi na kaka yake, Craig, walimpeleka kwenye mafunzo ya mchezo wa Judo.

Lakini alipokuwa na miaka 14, alitamani kujua michezo mingi zaidi ya mapigano kutokana na kukumbuka namna alivyoshambuliwa alipokuwa na miaka 13, tena alikuwa na mwalimu wake wa judo.

Hapo akaanza kujifunza mchezo mwingine wa mapigano maarufu Taekwondo kisha akajifunza Kickboxing, mchezo ambao alifanikiwa kuhitimu vyema mafunzo yake na akapata nafasi ya kuwa mkufunzi wa mchezo huo hadi leo.

Michezo mingine ya mapigano aliyojifunza Scott Adkins ni pamoja na ‘Ninjutsu’, ‘Karate’, ‘Capoeira’, ‘Jujutsu’, ‘Jeet’, ‘Kune Do’, ‘Krav Maga’, ‘Wushu’ na michezo ya kuweka mwili sawa.

Filamu zake za kwanza tangu alipojifunza mapigano tofauti ni filamu ya Kichina ya ‘Dei Seung Chui Keung’ (2001) alizoicheza Hong Kong ambapo waongozaji maarufu wa Hong Kong, Jackie Chan walimuona wakamtumia kwenye filamu zao hapo ndipo jina lake likazidi kujitangaza duniani kote.

Mwaka 2003 aliendelea na filamu mbalimbali za mapigano zenye mvuto mkubwa ikiwemo filamu ya ‘Special Forces’ na filamu ya ‘Assassination Games’ aliyocheza na mkali wa mateke, Jean-Claude Van Damme. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles