30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Scorpion alipata mafunzo ya karate kwa miaka saba

scorpion

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

MSHTAKIWA katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete (34) maarufu ‘Scorpion’, amekiri kupata mafunzo ya karate kutoka chuo cha mafunzo cha Ifakara mwaka 1989 hadi 1995.

Upande wa mashtaka katika kesi hiyo, umemuongezea mashtaka ya shambulilio kupitia kifungu namba 234 cha Sheria ya Makosa ya Jinai, ambacho kinaruhusu kuongeza au kubadilisha mashtaka.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Flora Haule, kwamba kesi hiyo imekuja mshtakiwa asomewe maelezo ya awali.

Katika maelezo hayo zaidi ya manane, mshtakiwa alikiri jina lake, sehemu anayoishi ambayo ni Machimbo Yombo na mafunzo hayo.

Hata hivyo, aliendelea kukana jina la Scorpion, mashtaka yake na kwamba hakukamatwa wala kuhojiwa na polisi kuhusu mashtaka hayo.

Wakili Katuga alidai kuwa Septemba 6, mwaka huu mshtakiwa alikuwa maeneo ya Buguruni Sheli na Septemba 12 alihojiwa na kukamatwa na polisi maelezo ambayo aliyakana.

“Mashahidi watakaotoa ushahidi katika kesi hii wapo sita. Upande wetu wa mashtaka utawasilisha vielelezo viwili, ikiwamo fomu namba tatu ya polisi (PF3) na ripoti ya daktari kuthibitisha mashtaka hayo,’’ alidai Katuga.

Hata hivyo, Hakimu Haule aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 14, mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa kusikilizwa.

Katika mashtaka yake, Njwete inadaiwa alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka huu maeneo ya Buguruni Sheli, Wilaya ya Ilala.

Inadaiwa kuwa aliiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 ukiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili ya mkononi na fedha taslimu Sh 331,000 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Said Mrisho.

Pia inadaiwa kuwa mshtakiwa kabla na baada ya wizi huo, alimchoma kisu machoni, tumboni na mabegani mlalamikaji huyo ili aweze kujipatia mali hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles