26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Maiti inayogombewa bado kizungumkuti

coffin2_2-jpgb9394da4-5103-4409-9c3b-07fbc28eeaf1original

Na KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

UAMUZI wa ubishani wa kisheria kuhusu mwili wa marehemu Ernest Materego uliokwama kuzikwa kwa zaidi ya siku 10, unatarajia kutolewa leo.

Mwili huo umekwama kuzikwa kwa sababu mdogo wa marehemu, mke na mtoto  wanabishania wapi mwili huo ukazikwe.

Juzi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam ilitoa amri ya muda kuzuia mwili usizikwe hadi shauri hilo limalizike.

Hata hivyo, wakati uamuzi huo unatolewa mwili ulikuwa njiani kuelekea Bunda.

Mwili huo ulifika Bunda na kuhifadhiwa hospitalini ukisubiri uamuzi wa mahakama.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba, jana alitakiwa kutoa uamuzi wa pingamizi la awali la kupinga mahakama hiyo kusikiliza shauri hilo kwa madai kwamba haina uwezo.

Wadai katika kesi hiyo ni mke wa marehemu, Joyce Materego na mtoto wake Edwin Materego wanaowakilishwa na Wakili Raymond Wawa wakati mdaiwa ni mdogo wa marehemu, Gonche Materego anayewakilishwa na Wakili Makaki Masatu.

Wakili Masatu aliwasilisha pingamizi akidai mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo kwa sababu inahusu masuala ya kimila, hivyo ifutwe.

Akijibu, Wakili Wawa alidai hoja iliyopo mahakamani si suala la kimila, bali wapi mwili wa marehemu ukazikwe, hivyo mahakama hiyo ina uwezo wa kusikiliza shauri hilo.

Hakimu aliahidi kutoa uamuzi jana ili shauri hilo liendelee kwa hatua nyingine, lakini hakuweza kufanya hivyo kwa sababu alikuwa hajamaliza kuandika.

Katika kesi hiyo, inadaiwa Materego alifariki dunia Novemba 19, mwaka huu na mkewe na watoto walitaka kuzika Dar es Salaam kwa sababu marehemu aliishi tangu mwaka 1974.

Mdaiwa akijibu, alidai marehemu alikuwa akiishi pia Bunda mkoani Mara, hivyo anatakiwa kuzikwa huko na si Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles