KUNDI la Sauti Sol kutoka nchini Kenya, juzi lilijikuta likishangazwa na idadi kubwa ya watu katika jiji la New York nchini Marekani, kabla ya onyesho lao katika ukumbi wa Central Park nchini humo.
Sauti Sol wako nchini Marekani kwa ajili ya tamasha la kimataifa la Global Citizen linalowakutanisha wasanii mbalimbali ambapo watu zaidi ya 60,000 wanakadiriwa walihudhuria tamasha hilo.
Tamasha hilo limeandaliwa kwa ajili ya kukuza elimu, kutetea haki za wakimbizi na kujadili mabadiliko ya hali ya hewa duniani, huku watu maarufu ambao waliongoza tamasha hilo ni pamoja na Bill Gates, Sir Richard Branson, Jay Z, Beyonce, Usher, Cold Play, Kerry Washington na wengine wengi.
“Ni mara yetu ya kwanza kuona ukumbi ukiwa umejaa kama hivi, hatuna uhakika kama tutapata nafasi ya kupanda kwenye jukwaa huku kukiwa na watu kama hawa,” walisema Sauti Sol.