30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SANGARA TANI 65.6 WAPIGWA MNADA

Na RENATHA KIPAKA-BUKOBA

SERIKALI imepiga mnada tani 65.6 za samaki aina ya sangara ambazo zilikamatwa katika Kisiwa cha Rubili Kata ya Mzainga wilayani Muleba mkoani Kagera, zikiwa zimevuliwa kwa njia haramu na kuziuza kwa Sh milioni 120.

Mnada huo ulifanyika juzi na umesimamiwa na Ofisa Kilimo na Udhibiti Ubora wa Mazao ya Samaki Mkoa wa Kagera, Monica Kishe, ikiwa ni agizo alilopewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, wakati wa  ziara yake ya siku mbili mkoani humo na kujionea hali halisi ya shehena iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ofisi za kituo cha ulinzi wa maliasili cha uvuvi mjini Bukoba.

Kishe alisema awali mnada huo uliahirishwa kutokana na kushushwa kwa bei elekezi ya Sh milioni 200 iliyokuwa imepangwa na Serikali  kuziuza hadi kufikia Sh milioni 70 zilizotamkwa na mnunuzi.

Alisema zoezi hilo lilisitishwa na kupatiwa maamuzi mapya kutoka  Ofisi ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi itolewe  bei ambayo itaendana na hali ya samaki ilivyo kwani samaki hao wakikaa muda mrefu hupungua uzito na kuendelea kuharibika.

“Tulivyoona sasa imeshindikana kufikia  bei tuliyopatiwa na Serikali, tulisitisha mnada na kusuburi maelekezo mengine kutoka kwa waziri mwenyewe,  tulimwambia madai ya wanunuzi ni  jinsi samaki walivyokaa muda mrefu tangu Desemba 30, mwaka jana hadi Januari 9, mwaka huu wanaendelea kuharibika na kupungua uzito,” alisema Kishe.

Naye Dalali wa Mahakama mkoani humo, Ignatus Bashemela, alisema hawakuweza kufikia lengo kwani wanunuzi walidai samaki hao wanaendelea kuharibika hivyo hawawezi kuwapatia faida kwenye masoko wanayotarajia kuuzia mzigo huo.

Kwa upande wake mnunuzi wa samaki hao kutoka Kata ya Izigo wilayani Muleba, Shafi Abdallah, alisema soko la samaki hao hupatikana nchini Congo kwani ndani ya nchi samaki walio na chumvi nyingi hushindikana kwa matumizi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles