24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

MWANAFUNZI ALIYEJAZWA MIMBA AFUNGWA MIEZI SITA

Na WALTER MGULUCHUMA, NKASI

AGATHA Mwananyau (19), aliyekatisha masomo akiwa kidato cha nne baada ya kupewa ujauzito, amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh 300,000.

Msichana huyo aliyekuwa akisoma katika Shule ya Sekondari Mkangale  katika Mji wa Namanyere wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa, aliacha masomo  baada ya kupewa ujauzito na Alfa Nestory (20).

Mshtakiwa huyo alishindwa kulipa faini  hiyo ambapo ameanza kutumikia adhabu  hiyo.

Juzi aliitwa na upande wa mashtaka kutoa ushahidi  katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi mbele ya Hakimu Ramadhani Rugemalira ambapo alitoa ushahidi wa uongo akisema aliyempatia ujauzito hakuwa mshtakiwa Nestory bali  alikuwa ‘mmachinga’ aliyetokea Mbeya  tofauti na maelezo yake ya awali.

Ndipo Mwendesha Mashtaka, Hamimu Gwelo, alipomshtaki kwa kutoa ushahidi wa uongo ambapo jana alifikishwa mahakamani hapo na aliposomewa mashtaka hayo alikiri kutenda kosa hilo.

Akitoa hukumu, Hakimu Rugemalira, alisema amezingatia utetezi wa mshtakiwa kuwa apunguziwe adhabu kwa kuwa ana mtoto mchanga mwenye umri wa miezi nane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles