27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

DIAMOND PLATNUMZ APEWE PONGEZI ZAKE

NA MWANDISHI WETU

UWEKEZAJI mkubwa kwenye tasnia ya habari na burudani unatarajiwa kufanywa hivi karibuni chini ya nyota wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ pamoja na kampuni yake ya Wasafi Classic Baby (WCB).

Tetesi za kufungua kituo cha redio na runinga zilizoibuka wiki mbili zilizopita, zimeanza kudhihirika katikati ya wiki hii baada ya mkali huyo wa muziki (Diamond Platnumz), kuweka wazi video inayoonyesha makao makuu ya kampuni hiyo.

Mjengo huo wa ghorofa moja uliopo maeneo ya Mbezi Beach, Dar es Salaam alitangaza kuwa utakuwa makao makuu mapya ya lebo ya WCB badala ya yale yaliyopo Sinza, huku vitengo vyake kama studio ya kurekodi muziki na picha, studio ya filamu, wasafi.com na Wasafi Fm, Wasafi Tv zikihamishiwa humo.

Pongezi kutoka sehemu mbalimbali zimemiminika kwa Diamond Platnumz na uongozi wake chini ya mameneja, Babu Tale, Sallam Sk na Mkubwa Fella kwa kumfanya mwanamuziki huyo kuwekeza nje ya muziki.

Huu unaweza kuwa uwekezaji mkubwa zaidi kuwahi kufanywa na msanii wa Bongo Fleva kwenye sekta ya habari na burudani, inapendeza na inaamsha ari kwa vijana wengine wenye vipaji walio mtaani.

Hasa pale anapomtazama Diamond Platnumz kutoka  Tandale mpaka Diamond huyu anayetoa ajira kwa vijana wengi kupitia bidhaa zake na shughuli nyingine kubwa zilizofanikiwa kupitia mgongo wake.

Inafahamika kuwa kupitia yeye wasanii kama Harmonize, Rayvanny, Lavalava na mpiga picha maarufu (Kifesi), wamefahamika na kupitia muziki wanaofanya unasaidia kundi jingine kubwa la watu walio nyuma yao.

Katika zama hizi tunazoishi chini ya kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda uwekezaji kama huo unaofanywa na Diamond Platnumz, unapaswa kupongezwa na si kubezwa kwa lengo la kumrudisha nyuma.

Ushabiki uwekwe pembeni, hizi ni juhudi ambazo tunahitaji kuziona kwa wasanii wengine wa hapa nchini, tunahitaji kuwaona kina Diamond wengine wengi wakifanya uwekezaji na kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania.

Tuondoe tofauti zetu zinazozalisha chuki na kufanya tuwe na tabia ya kutaka kumshusha fulani ili kumpandisha mtu fulani na kusahau kuwa wote wawili au zaidi wakiwa juu tutanufaika sote na sekta yetu ya sanaa itakua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles