28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

AZAM AU URA KOMBE LA MAPINDUZI?

Na SAADA SALIM -ZANZIBAR

TIMU ya Azam FC leo itakuwa inacheza fainali ya kihistoria ya Kombe la Mapinduzi katika Uwanja wa Amaan mjini hapa kwa kumenyana na URA ya Uganda.

Mchezo huo utakaochezwa saa 2:15 usiku, unaipa Azam nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kutokana na kuwa bingwa mtetezi.

URA wameongoza Kundi A baada ya kushinda mechi tatu na sare moja, wakati Azam wakifuatia kwa kupoteza moja mbele ya timu hiyo huku wakishinda michezo mitatu.

Azam katika mchezo wa leo itakuwa na kibarua cha kutetea ubingwa huo huku pia kulipa kisasi cha kufungwa na URA bao 1-0 katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Azam inanolewa na kocha Mromania, Aristica Cioaba, wakati URA ikinolewa na kocha mzawa, Ntaka Paul.

Makocha hao walijinadi kila mmoja akiamini kikosi chake kipo vizuri na tayari kwa ajili ya kutwaa taji hilo la ubingwa wa Mapinduzi.

Cioaba alisema wamejiandaa na sasa kilichobakia ni vijana wake kwenda kumaliza kazi.

“Tumefika hapa kutokana na maandalizi na timu nzima kujituma, tunajua mechi ya fainali ni ngumu zaidi kwa kuwa URA watakuwa na mbinu tofauti, tupo tayari kwa ajili ya kutetea taji letu,” alisema.

Wakati huo huo kocha wa Uganda, Ntaka, alisema haoni jipya la wapinzani wake hao kwani anaamini kilichotokea katika makundi kitajirudia tena.

“Azam nimeifunga ila sitabweteka, nimejipanga na kuhakikisha tunaingia na mbinu mpya ili tuondoke na kombe kama ilivyokuwa 2016,” alisema.

Azam ndio wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano hiyo baada ya timu zote za Tanzania Bara na Zanzibar kung’olewa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles