27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

PLUIJM AITOLEA MACHO SIMBA

Na SAADA SALIM –ZANZIBAR

KOCHA mkuu wa Singida United, Hans Pluijm, ameanza kuipigia hesabu timu ya Simba ya kuhakikisha inaing’oa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba iliyo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 26, itamenyana na Singida United Januari 18, mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA, Pluijm alisema michuano ya Kombe la Mapinduzi imewapa mazoezi tosha kwa ajili ya kuivaa Simba.

“Hii michuano ilinipa nafasi ya kuwasoma wapinzani wangu, pia imewafanya wachezaji kupata mazoezi kuikabili Simba,” alisema Pluijm aliyewahi kuifundisha Yanga.

Alisema ameona Simba inavyocheza na kujua mbinu zao na kwamba lengo lao ni kuhakikisha wanawashusha kileleni.

Alisema anahitaji kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo wakiwa katika nafasi ya pili au kukaa kileleni mwa msimamo huo ili waweze kutimiza ndoto zao za kutwaa ubingwa.

Alisema ameona mfumo ambao unatumiwa na Simba chini ya kocha wao, Masoud Djuma na kwamba anaufanyia kazi kuhakikisha wanafikia lengo lao la kupata pointi tatu.

Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 26 sawa na Azam FC wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga, huku Singida wao wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na pointi 23.

Singida United iling’olewa na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi Jumatano iliyopita kwa kufungwa bao 1-0.

Bao hilo lililoipa Azam nafasi ya kutinga fainali, lilifungwa katika dakika ya 78 na Shaaban Idd Chilunga, kwa shuti lililomshinda kipa wa Singida, Peter Manyika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles