27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

BUNGE LAKUSUDIA KUPUNGUZA GHARAMA VIKAO VYA KAMATI

Na GRACE SHITUNDU

KAMATI za kudumu za Bunge zinatarajiwa kuanza vikao vyake mjini Dodoma Jumatatu ijayo, huku vikao hivyo sasa vikifanyika katika kumbi za Ofisi ya Bunge mjini Dodoma ili kuepuka ukubwa wa gharama.

Imeeleza kwamba, shughuli za kamati hizo zitafanyika katika kumbi za Ofisi ya Bunge ili kuepuka ukubwa wa gharama kwa kukodi kumbi nje ya Ofisi ya Bunge.

Pia Bunge linalenga kuondoa usumbufu kwa wabunge kutokana na umbali wa kumbi zilipo, ugumu wa uratibu kutokana na kutawanyika kwa kumbi na usumbufu kwa wadau wanaoalikwa kwenye kamati na changamoto ya utoaji wa huduma muhimu zinazofanikisha shughuli za kamati.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na    Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano cha Bunge, shughuli hizo zitaanza Januari 15 hadi 27 kabla ya kuanza mkutano wa kumi wa Bunge unaotarajiwa kuanza Januari 30, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba, kamati tatu ambazo ni Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, zitafanya ziara za ufuatiliaji katika maeneo mbalimbali nchini.

Kamati hizo pia zitafanya uchambuzi wa miswada mbalimbali na kupokea maoni ya wadau wanaoguswa na miswada husika.

Imeeleza kamati nyingine tatu zitafanya uchambuzi wa miswada ya sheria ambapo Kamati ya Katiba na Sheria itachambua na kujadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Na. 5 wa mwaka 2017 pamoja na kupokea maoni ya wadau Januari 16.

 “Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii itachambua na kujadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Hifadhi ya Wanyamapori ya mwaka 2017, itapokea maoni ya wadau Januari 16.

“Kamati nyingine ni Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambayo itachambua Muswada wa Sheria ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2017 na itakuwa na vikao vya kupokea maoni ya wadau Januari 18,” ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo pia imeeleza katika vikao hivyo kamati tisa za kisekta zitaendelea kupokea taarifa za kiutendaji wa Wizara zinazosimamiwa na Kamati hizo kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (1) (c) na (d) cha nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo Januari, 2016.

Aidha, Kamati ya Bajeti pamoja na shughuli nyingine itapokea maoni ya wadau wa utalii kuhusu mwenendo wa shughuli za utalii baada ya kuanzisha utozaji wa VAT kwenye shughuli za utalii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles