24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

MWEKEZAJI AWAMEGEA ENEO WACHIMBAJI WADOGO

Na FREDRICK KATULANDA-MISUNGWI

KAMPUNI ya Madini ya Carlton Kitonga (T) Ltd, imetoa sehemu ya eneo lake la hekta sita kwa ajili ya uchimbaji wa dhahabu kwa wachimbaji wadogo wa Kikundi cha Buhunda kilichopo Ishokelahera Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Meneja Mkazi wa Kampuni ya Rift Valley Resources ambayo ni Kampuni mama ya Carloton Kitonga, Bartolomeo Mkinga, alisema wamefikia uamuzi wa kumega sehemu ya eneo lao kwa wachimbaji wadogo, licha ya kulimiliki kihalali na wamekuwa wakilifanyia utafiti kwa muda wa miaka 12.

Alisema eneo hilo wamekuwa wakilifanyia utafiti kutoka mwaka 2006 na kubainisha kuwa katika kipindi hicho wametumia kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 10.8 hivyo kudai kuwa wametoa eneo lenye madini kwa wachimbaji hao na wao kubakiwa na eneo lingine kubwa ambalo wataendeleza shughuli zake bila ya kuingiliana na wachimbaji wadogo.

Alisema kwa muda wamekuwa katika mgogoro na wachimbaji wadogo kuvamia eneo ambalo wao wamekuwa wakilimiliki kihalali, hivyo kulazimika kutumia gharama kubwa za kulilinda lisivamiwe, lakini kufuatia mazungumzo baina yao, wachimbaji wadogo chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, wameamua kutoa eneo hilo ili kumaliza migogoro ya kuvamiwa kila mara.

“Tulijadiliana kwa pamoja na Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa na tayari tumesaini mkataba wa makubaliano kwa ajili ya kuwapatia eneo hilo, kilichobaki ni kukamilisha mchakato wa utoaji wa leseni kwa Buhunda ili walimiliki kisheria,” alisema.

Alisema katika makubaliano yao, Kikundi cha Buhunda kitawajibika kusimamia wachimbaji wadogo kufanya kazi katika eneo walilopewa kuepusha uvamizi wa eneo lingine la mwekezaji Calton Kitonga kuvamiwa na wao wakiwa na wajibu wa kuandika barua kwa Kamishna wa madini ili kuruhusu wapewe leseni ya umilikaji na kuanza uchimbaji.

Kwa upande wake Katibu wa Kikundi cha Wachimbaji wa Buhunda, Casmir Chahe, alisema wamepokea kwa furaha hatua hiyo na kuahidi kusimamia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles