24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

NIGERIA WAPANIA KUTWAA UBINGWA CHAN

RABAT, MOROCCO

MICHUANO ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani (Chan), yanatarajia kuanza leo nchini Morocco, huku timu ya Taifa ya Nigeria ikipania kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza.

Uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kwamba maandalizi yao yamekwenda vizuri na wanaamini wana nafasi kubwa ya kurudi na taji hilo, hivyo wamedai huu ni wakati wa wasanii wa muziki nchini Nigeria kuanza kuandaa nyimbo kwa ajili ya kusherehekea ubingwa huo.

Viongozi hao wamedai kwamba timu hiyo ilishindwa kufanya vizuri kwa miaka iliyopita kutokana na kukosa michezo mingi ya majaribio, lakini safari hii wamefanikiwa kuipata hivyo wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Kocha wa timu hiyo, Salisu Yusuf, amesema kwa sasa ana uzoefu wa kutosha katika michuano hiyo, hivyo hana wasiwasi kwa kuwa ana wachezaji wenye uwezo mkubwa kama vile nahodha, Ikechukwu Ezenwa, Stephen Eze, Kalu Orji Okagbue na Rabiu.

“Sina wasiwasi na kikosi nilichokuwa nacho, wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na wananipa matumaini ya kurudi na taji, ninajua ushindani wa michuano hii, hivyo maandalizi yetu yatatubeba kwa kiasi kikubwa.

“Kikubwa ni kwamba, wasanii wa nchini Nigeria waandae nyimbo za kuishangilia timu yao mara baada ya kutwaa ubingwa,” alisema Yusuf.

Timu hiyo ya Nigeria inatarajia kutupa karata yake ya kwanza Jumatatu dhidi ya wapinzani wao Rwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles