27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Sanga alia na mkandarasi wa umeme Makete

Na Mwandishi Wetu, Makete

Mbunge wa Makete, Festo Sanga amesema Mkandarasi aliyepewa tenda ya kusambaza umeme wilayan humo bado afanyi vizuri kwani bado vitongoji vingi havina umeme na kata zaidi ya nne bado havijafikiwa na nishati hiyo muhimu.

Sanga ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, Desemba 19, baada ya malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Ndapo kata ya Kinyika wilaya ya Makete mkoa wa Njombe ambao wameiomba serikali na mbunge wao kuharakisha kufikisha umeme katika taasisi muhimu za umma kama shule, hospital na makanisa ili kufanya watoa huduma wakiwemo walimu kushawishika kufika katika kijiji hicho kufanya kazi.

Kwa mujibu wa wananchi hao kwa sasa baadhi ya walimu wakipangiwa katika kijiji hicho wanakataa kwenda kufundisha kwa sababu hakuna umeme.

“Nimepokea changamoto ya wananchi kuhusu ukosefu wa umeme, na changamoto hapa inakuja kwamba mkandarasi aliyepewa tenda ya kusambaza umeme wilayani hapa bado afanyi vizuri kwani bado vitongoji vingi havina umeme na kata zaidi ya nne bado havijafikiwa na nishati hii.

“Hivyo mimi kama mbunge nimelibeba hili na nitafikisha kero hii kwa waziri wa Nishati (Dk. Medard Kalemani) kuona atakavyosaidia ili mkandarasi aende haraka kusambaza umeme kwani makao makuu ya kijiji kua na umeme bila vitongoji si sawa kwani hamna kijiji bila kitongoji,” amesema Sanga.

Upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya shule ya Msingi ya Iwale, Asifiwe Mahenge amesema wanaomba sana umeme ufike katika sehemu hizo za taasisi kwani bila kufika wanakosa walimu kufika hapo.

“Walimu wanauliza kuna umeme shule hiyo ili niende,tukisema umeme haupo basi anaamua kwenda kwenye shule zingine ambazo umeme upo tunaomba mbunge na diwani watusaidie umeme ufike shule ya msingi Iwale na sekondari ya Kinyika,” amesema Asifiwe.

Naye Msimamizi wa Mradi wa REA kwa wilaya ya Makete, David Jekela ametolea ufafanuzi sababu ya nguzo za umeme kutofika katika taasisi za umma ni kwasababu mpimaji hakufanya kazi yake vizuri.

Amesema kuna sehemu eneo la kazi kaweka nguzo zifike lakini katika ramani ambayo yeye amekabidhiwa na mkandarasi wa mkoa hazipo hivyo kufanya nguzo alizopewa zisifike sehemu muhimu na hivyo anamalizia kupima tena ili afikishe ni nguzo ngapi zinatakiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles