31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Askofu akemea dawa za kulevya, ngono vyuoni

Na Safina Sarwatt, Moshi

Askofu wa Jimbo Katoliki la Same mkoani Kilimanjaro, Mhashamu Askofu Rogath Kimario amekemea vitendo vya matumizi ya dawa za kulevya na mahusiano ya kingono katika vyuo vikuu nchini na kwamba kujihusisha na vitendo hivyo ni dalili ya kutojitambua.

Askofu Kimario ametoa onyo hilo leo Desemba 19, katika mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mwenge ambapo Jumla wahitimu 1,762 wa fani mbalimbali wamehitimu masomo yao.

Amesema mahusiano ya kingono na matumizi ya dawa za kulevya imekuwa changamoto katika vyuo vikuu hapa nchini, na kwamba taifa linatakiwa kusimama na kukemea vitendo hivyo.

“Kujihusisha na vitendo hivyo ni dalili mbaya kwa wasomi wa vyuo vikuu hivyo badilikeni jisahihisheni msioneane aibu, tunataka taifa yenye maadili mema,” amesema Askofu Kimario.

Amesema taifa linahitaji wasomi waadilifu wenye uwezo na wabunifu hivyo kujiingiza katika mambo ya ovyo nikupotenza dira ya maisha.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mwenge, Prof. Philbert Vumilia amesema uhitaji wa wasomi kwa sasa ni mkubwa sana hivyo kuwataka wahitimu kujituma ili kuchochea maendeleo katika jamii.

“Msitafute vyeti kwa ajili ya kutafuta kazi bali itumie elimu kuinufaisha jamii, kuweni wabunifu katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo,” amesema Professa Vumilia.

Prof. Vumilia amewataka wahitimu hao kutambua wanamchango mkubwa katika taifa hili hivyo watumie elimu waliyopata kufanya utafiti wa masuala mbalimbali .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles