NYOTA wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Cameroon, Samuel Eto’o, amefanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Georgette Tra Lou.
Harusi hiyo ilifungwa katika kanisa kuu la mjini Stezzano nchini Italia, huku nyota wengi wa soka wakijitokeza katika sherehe hiyo ambayo ilifanyika juzi.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, inadaiwa kwamba alifunga ndoa na mrembo huyo tangu mwaka 2007, lakini hawakuvaa nguo maalumu kwa ajili ya harusi, hivyo juzi waliamua kuifanya sherehe ya wazi huku wakivaa nguo hizo.
Wawili hao tayari wana watoto wawili katika maisha yao ya pamoja. Katika sherehe hiyo nyota wa zamani wa klabu ya Barcelona ambaye alikuwa anacheza nafasi ya ulinzi, Carles Puyol aliungana na wachezaji mbalimbali.
Eto’o kwa sasa anakipiga katika klabu ya Antalyaspor ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Uturuki.