27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Carlos Dunga atimuliwa

Carlos Dunga
Carlos Dunga

RIO DE JENAIRO, BRAZIL

BAADA ya timu ya Taifa ya Brazil kuondolewa kwenye michuano ya Copa America nchini Marekani katika hatua ya makundi, Brazil imeamua kumfukuza kocha wake, Carlos Dunga.

Kocha huyo ambaye zamani alikuwa ni mchezaji wa timu hiyo, ametimuliwa kwenye nafasi yake kufuatia nchi hiyo kutupwa nje ya michuano hiyo dhidi ya Peru.

Shirikisho la Soka la Brazil, CBF, limetoa taarifa ya kumtimua Dunga ambaye pia alitarajiwa kuiongoza nchi hiyo kwenye michezo ya Olimpiki ambayo itachezwa nchini humo Agosti mwaka huu.

Pamoja na Dunga, pia wasaidizi wake wote wa benchi la ufundi wameondolewa katika kikosi hicho na CBF imesema itateua watu wengine kuiongoza timu hiyo.

Brazil ilifungwa bao 1-0 na Peru, linaloelezwa kuwa la mkono, hii ni historia kwa mara ya pili kati ya miaka 100 katika mashindano hayo kushindwa kuvuka hatua ya makundi.

Dunga ambaye alikuwa nahodha wa Brazil mwaka 1994 walipobeba Kombe la Dunia, aliteuliwa kuwa kocha wa Brazil kwa mara ya kwanza mwaka 2006, lakini alifukuzwa mara baada ya kuchapwa na Uholanzi kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini, alitajwa tena kuwa kocha mkuu baada ya nchi hiyo kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 zilizochezwa kwao Brazil na akachukua nafasi ya Luiz Filipe Scolari.

Lakini tangu atwae wadhifa huo, ikiwa ni mara yake ya pili kuwa kocha wa Brazil, nchi hiyo haijafanya vyema na kutolewa nusu fainali ya Copa America ya 2015 kwa penalti na Paraguay ambayo ilifanyika nchini Chile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles