
NEW YORK, MAREKANI
MSANII wa muziki na filamu nchini Marekani, Miley Cyrus, amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, Liam Hemsworth.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo mwenye umri wa miaka 23, ameweka picha ya pete hiyo na kudai kwamba ina thamani ya dola 100,000, akiwa amevishwa na mpenzi wake huyo mwenye umri wa miaka 26.
“Nadhani hii ni sehemu ya awali katika kuyaandaa maisha yangu, haina maana kwamba nataka kuolewa leo au kesho nadhani muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi.
“Kwa sasa najiona nina umri mdogo, bado nina mambo mengi ya kuyafanya kabla ya kupata watoto, lakini kila kitu kina wakati wake,” aliandika Miley.