22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Samia aitupia dongo Wilaya ya Hai

Bi.-Samia-SuluhuPatricia Kimelemeta na Omary Mlekwa,Hai

HALMASHAURI ya Wilaya ya Hai imedaiwa kuwa miongoni mwa wilaya zinazoongoza kwa kupokea na kutoa rushwa, hali iliyosababisha baadhi ya miradi ya maendeleo kukwama.
Hayo yalibainishwa na mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Foo, Kata ya Machame Kaskazini.
Alisema fedha za miradi ya maendeleo zilizokuwa zinatolewa na Serikali hazijatumika kwa malengo yaliyokusudiwa jambo ambalo limesababisha kujitokeza kwa malalamiko.
“Tumepata taarifa kuwa baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai siyo waadilifu, wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa jambo ambalo limesababisha kukwamisha maendeleo,” alisema Samia.
Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali itawachukulia hatua watendaji hao na wale watakaobainika wanaendelea na vitendo hivyo ili iwe fundisho kwa wengine.
“Mkakati wa Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha wanakarabati mahakama ya mwanzo ya Masama Kati ili iweze kutimiza majukumu yake katika mazingira mazuri,” alisema.
Alisema mkakati mwingine ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara ikiwamo Barabara ya Kialia, Sadala Masama ambayo tayari ujenzi umeanza ambayo inatekelezwa kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete.
Samia alisema katika ilani ya CCM wamepanga kuboresha sekta ya elimu ikiwamo ujenzi wa maabara pamoja na kuziwekea vifaa vyake, mabweni na kuongeza vyumba vya madarasa pamoja na upatikanaji wa vitendea kazi katika shule mbalimbali nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles