27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Bashe: Uchaguzi huu ni mgumu

Hussein-BasheNa Odace Rwimo, Nzega

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mjumbe wa mkutano mkuu CCM taifa, Hussein Bashe, amewaambia wanachama wenzake kukaza buti kwani uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu.
Bashe alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wenzake pamoja na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho wilayani Nzega.
Alisema wanaCCM wanatakiwa kutambua kuwa uchaguzi wa mwaka 1995,2000,2005,2010 na huu wa 2015 kuna tofauti kubwa, hivyo wanatakiwa
kujipanga.
Bashe aliyepitishwa na CCM kuwania ubunge Jimbo la Nzega, alisema uchaguzi utakuwa rahisi zaidi endapo kutakuwa na majibu sahihi ya kero za wananchi zinazowakabili.
“WanaCCM tunapaswa kutambua tuna kazi kubwa kuhusiana na uchaguzi wa mwaka huu. Hapa hakuna kubweteka, tunatakiwa kufanya kazi za ziada na kuwaeleza wananchi juu ya kero zinazowakabili,”alisema.
Akizungumzia uhakiki wa wananchi kujiandikisha, Bashe alisema haiwezekani kuwa na uchaguzi wakati wananchi watakuwa hawajajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura.
Alisema kujiandikisha na kupiga kura ni haki ya mwananchi, hivyo kila mwananchi anapaswa kuhakikiwa ili haki hiyo isipotee.
Bashe alisema kuwepo uchaguzi wakati baadhi ya wananchi hawaoni majina yao wakati walijiandikisha ni kuminya haki hiyo.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Abrahaman Mdeme, alitoa ufafanuzi juu ya mashine za BVR kuendelea kufanya kazi katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo.
Mndeme alisema ni kweli kuna maeneo kuna uhakiki wa majina ya wananchi kama wale ambao picha hazionekani, taarifa zilikosewa na uhakiki hufanyika na kupatiwa vingine.
Alisema maneno ya baadhi ya watu kudai uandikishaji huo ni sehemu ya mkakati wa bao la mkono ni uzushi tu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles