24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Samia ahimiza uwezeshwaji wanawake

Samia Suluhu HassanNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAKAMU wa Rais,  Samia Suluhu Hassan,  amehimiza wanawake wajasiriamali   Tanzania Bara na Visiwani kujiunga na majukwaa ya kuwezesha wanawake katika uchumi yatakayoanzishwa nchini kwa ajili ya kuwapatia elimu ya ujasiriamali.

Aliyasema hayo Dar es Salaam jana  alipofungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) JKT Mgulani.

Alisema kama wanawake watayatumia majukwaa hayo ya  uchumi  watakuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa bora, kutafuta masoko, kupanga bei nzuri za bidhaa na kupata fursa za mikopo.

Makamu wa Rais  aliwataka wanawake wajasiriamali kuichukulia ajira hiyo kama ajira yo yote rasmi kwa kuwa serikali itaweza tu kutimiza azma yake ya kupunguza ukosefu wa ajira kupitia sekta ya viwanda vidogo ambavyo vingi vinaendeshwa na wajasiriamali.

“Kupitia majukwaa niliyoyataja ya kumwezesha mwanamke katika uchumi nitajihidi kuhakikisha  majukwaa haya yanatoa majibu ya changamoto zinazowakabili wanawake wajasiriamli na kuchangia ukuaji wa ajira, kuondoa umaskini na kuwezesha ujenzi wa taifa la viwanda,” alisema.

Mwenyekiti wa EOTF, Mama Anna Mkapa,  alisema tangu Mfuko huo uanzishwe miaka 19 iliyopita umetoa mafunzo kwa zaidi ya wanawake wajasiriamali 30,000 na umewezesha wajasiriamali 14,500 kushiriki maonyesho ya Sabasaba ili kutangaza na kuuza bidhaa zao.

“Wanawake hawa wamejenga nyumba bora, kusomesha watoto, kulipia huduma za matibabu, shughuli za  familia kutokana na mafanikio ya biashara zao zilizoborehwa na mafunzo hayo,” alisema Anna.

Mama Mkapa alimwahidi Makamu wa Rais kuwa mfuko huo utaendelea na jitihada zake za kutoa elimu kwa wanawake wajasiriamali na kuwawezesha kushiriki katika maonyesho ya biashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles