23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Magazeti ya Serikali yapata bosi mpya

JimYonaziNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli amemteua Dk. Jim Yonazi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi jana, ilieleza kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kuanzia Juni 18, mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo, Dk.   Yonazi alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Dk.   Yonazi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Gabriel Nderumaki ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Aprili 14, mwaka huu, Rais Magufuli, alitengua uteuzi wa Nderumaki  na kumteua Tuma Abdallah kukaimu nafasi hiyo.

Hatua hiyo ilitokana na uamuzi wa bodi ya TSN iliyokutana Februari 22, mwaka huu,  kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo, ikiwa ni muda mfupi baada ya ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye aliyetembelea  kampuni kuangalia jinsi ya kuboresha utendaji   kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles