28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

SAMIA AAGIZA WENYE MADENI YA PEMBEJEO WASHUGHULIKIWE

NA FLORENCE SANAWA, GRACE SHITUNDU

MAKAMU  wa Rais  Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango kuhakikisha wanaohusika na madeni ya pembejeo wanafikishwa katika Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) ili wachukuliwe    hatua.

Alikuwa akizungumza wakati akifunga maonyesho ya Nanenane   katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi jana.

Samia alisema   rasimu ya kwanza ya ripoti ya madeni ya pembejeo ilionyesha kuna watu wanawahujumu wakulima.

Alisema baada ya Serikali kukamilisha uhakiki wa madeni ya wazabuni wa pembejeo imebaini kuwapo   unyonyaji mkubwa kwa wakulima hali ambayo imechangia kuwadhoofisha.

“Hatuwezi kuendelea kulinda watu ambao kwa makusudi walikuwa wakihujumu taifa, kilimo na wakulima kwa faida yao.

“Wananyonya jasho la wakulima, hatua zichukuliwe… nione Wizara ya Kilimo imefanya jambo kuwashughulikia watu hao.

“Katika jambo hili sitakuwa yule mliyemzoea, nitabadilika na kutaka kuona hatua madhubuti zimechukuliwa dhidi yao na wakulima wanapata stahiki yao,” alisema Suluhu.

Alisema baada ya Serikali kukamilisha uhakiki wa madeni ya wazabuni wa pembejeo hali siyo nzuri kwa kuwa wamegundua kiasi kikubwa cha udanganyifu na zipo mbinu nyingi wanazotumia  pembejeo zisiwafikie wakulima  wala kutoshirikishwa kamati zinazohusika.

Alisema suala la ugawaji wa pembejeo wakulima wanapoambiwa wajiandikishe wajue Serikali inataka kuwafanyia jambo.

Makamu wa rais aliagiza wakulima   nchini kuitumia Benki ya Wakulima kupata  mikopo.

“Hii ni benki yenu itumieni ipasavyo  muweze kunufaika, nimekuwa shahidi baada ya kuona wakulima walioweza kunufaika na benki hii wakiendelea vizuri,”alisema.

Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba alisema    wapo wakulima wameshindwa kupulizia dawa kwenye mashamba yao kwa kuwa walikosa dawa ya sulphur.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles