23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

SAKATA LA NONDO


*AG, DCI waitwa mahakamani

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, leo inatarajia kuwasiliza maelezo ya ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) pamoja na Mwanasheri Mkuu wa Serikali kuhusu shauri la dhamana ya mwanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Abdul Nondo.

Uamuzi huo wa mahakama huenda ukategua kitandawili cha hatima ya dhamana ya mwanafunzi huyo ambaye anashikili na Jeshi la Polisi kwa siku ya 15 sasa bila kufikishwa mahakamani.

Wiki iliyopita, mawakili wa Mtandao wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC), Mtandao wa Wanafunzi (TSNP) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu waliwasilisha maombi Mahakama Kuu kuitaka itoe amri kwa Jeshi la Polisi kumpeleka Nondo mahakamani au kumpa dhamana wakati shauri la msingi likiwa linaendelea.

Katika shauri hilo ambao litasilikizwa leo na Jaji Rehema Sameji, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI) wakitarajiwa kuwasilisha maelezo yao mahakamani hapo.

Nondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa  Wanafunzi Tanzania (TSNP), alitoweka katika mazingira ya kutatanisha Machi 6, mwaka huu na kupatika Mafinga mkoani Iringa

Nondo, ambaye pia Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), anadaiwa kutoweka muda mfupi baada ya kuandika kwenye mtandao kwamba yupo hatarini.

Inaelezwa kuwa Nondo alianza kujitoa kwenye makundi hayo Machi 7, mwaka huu kati ya saa 6:00 na 8:00 usiku jambo ambalo liliwashangaza na kuwapa shauku ya ….

Pamoja na hali hiyo jana mawakili Nondo, alijikuta katika wakati mgumu na kukimbilia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusubiri huenda mwanafunzi huyo angefikishwa katika mahakama hiyo.

Wakili Jones Sendodo, alisema kuwa kwamba walifika kituoni na kuelezwa kuwa, Nondo hayupo kituoni hapo.

“Tulienda kwenye Ofisi ya Kamanda Mambosasa (Lazaro Mambosasa-Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam), tumeambiwa yupo kwenye kikao.

“Tumepiga simu zake, hapokei. Hata hivyo, Kamanda Mambosasa amekuwa akitukwepa na kuwaambia waandishi kuwa sisi tunaishia mapokezi kitu ambacho sio cha kweli,’’ alisema Sendodo.

Alisema wakati wote mawakili wa LHRC wamekuwa wakipamba ili Nondo apate haki ya kikatiba ya kupata dhamana.

Taarifa zilizopatikana jana jioni wakati tukienda mtambaoni, zilieleza kwamba uongozi wa (Daruso) chini ya Rais wake Jilili Jeremiah walikwenda Kituo Kikuu cha Polisi na barua za kumdhamini Nondo bila mafanikio.

Huku wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu kiendelea kupambana kuhusu dhamana Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo apelekwe mahakamani, baba mzazi wa mwanafunzi huyo, Omar Nondo, ameiomba Serikali isimdhuru mtoto wake kwani ndiye anayemtegemea.

Baba mzazi wa mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alitoweka Machi 6, na akaonekana Machi 7 mjini Mafinga, wilayani Mufindi, mkoani Iringa alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na chombo kimoja cha habari (si MTANZANIA).

Baada ya Nondo kuripoti polisi Mafinga, Jeshi la Polisi mkoani Iringa lilisema kuwa ameripoti kuhusu kutekwa na kwamba limefungua faili kuchunguza.

Licha ya hali hiyo baada ya kusafirishwa na kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema kupitia uchunguzi wa kisayansi wamebaini kuwa Nondo hakutekwa bali alijiteka na kwamba alikwenda Mafinga kwa mpenzi wake.

Mpaka jana Nondo, alikuwa anashikiliwa na polisi huku wenzake wanne wa TSNP wakiwa wameitwa na kuhojiwa katikati ya wiki.

Licha ya kukaa polisi siku 15, Nondo bado hajapewa dhamana na anashikiliwa na Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam.

Baba wa mwanafunzi huyo, Omar Nondo alisema kama wameona mwanaye ana kosa basi ni vyema wamfikishe mahakamani ili aendelee na masomo kwa kuwa kosa lake lina dhamana.

Hata hivyo alisema inaonekana kwa sasa mtoto wake anahukumiwa kabla ya kufikishwa kwenye chombo cha mwisho cha maamuzi na mbaya zaidi anashikiliwa bila hata kupata muda wa kutoa maelezo wa namna tukio hilo lilivyokuwa.

TAMKO LA NONDO

Februari 18, mwaka huu Mwenyekiti wa mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo , alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi,  Dk. Mwigulu Nchemba kujiuzulu kutokana kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji  cha Taifa (NIT).

“Tunamuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, ajiuzulu kwa sababu ameshindwa kusimamia nafasi yake na kuangalia mienendo ya Jeshi la Polisi ambapo kila siku matukio yanatokea.

“Haya matukio yamekuwa yakishamiri sana ambapo yalianzia kwa wanasiasa, ambapo tulikuwa tukiyasikia haya matukio hadi kwa wanafunzi na watu wasiokuwa na hatia,” Nondo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles