28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Saida Karoli, Kingwendu kutumbuiza ‘mateja’ Moro

Saida Karoli..NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

MSANII maarufu nchini, Saida Karoli na msanii waliyewahi kugombea ubunge jimbo la Kisarawe kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Rashid Mwinshehe, maarufu ‘Kingwendu’, wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la kuunganisha nguvu za jamii kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana.

Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Desemba 20, limeandaliwa na viongozi wa dini wa Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Kampuni ya Beula Communications, lengo likiwa ni kuwapa matumaini vijana waliokuwa wanatumia dawa za kulevya na kuamua kuacha.

Akizungumzia tamasha hilo, Mkurugenzi wa Beula Communications, Melkezedek Mutta, alisema mbali ya Saida, pia Msanii mkongwe na mwenye vituko lukuki, Rashid Mwinshehe, maarufu Kingwendu, kwaya mbalimbali kutoka Dar es Salaam pamoja na kikundi cha Kaswida cha mjini Morogoro watanogesha tamasha hilo.

Alisema katika tamasha hilo, wataendesha harambee ambayo itasaidia kujenga kituo maalumu kwa ajili ya kuwakusanya na kuwapa stadi za maisha, ukiwamo ujasiriamali vijana walioathiriwa na dawa za kulevya kutokana na wengi wao kutokuwa na ujuzi wowote.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo anatarajiwa kuwa Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles