24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

SAFARI YA LISSU KWENDA ULAYA YAIVA

Na ASHA BANI -DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, anaendelea vizuri kutokana na kumaliza awamu zote za upasuaji.

Mbowe alisema hayo jana wakati akijibu maswali kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliotaka kufahamu maendeleo ya Lissu kwa sasa.

Mbowe alisema kuwa amemaliza awamu zote za upasuaji katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya na ameanza mazoezi ya viungo.

“Kubwa tunamshukuru Mungu Lissu ameweza kukaa mwenyewe na sasa amemaliza awamu zote za matibabu na Jumamosi ya Junuari 6, mwaka 2018 anakwenda nchi za Ulaya ingawa siwezi kutaja nchi kwa sasa kwa sababu za kiusalama ila akifika ndiyo nitaisema.

“Na ninachoweza kusema mpaka sasa gharama za matibabu mheshimiwa Tundu Lissu yamegharimu Dola za Marekani 300,000.

“…hadi sasa Serikali, Bunge hawajatoa chochote japo waliahidi kufanya hivyo,” alisema Mbowe.

Alipoulizwa kuhusiana na Lissu kubaki na risasi katika mwili wake, alisema hilo ni suala la kitabibu hawezi kulizungumzia lakini anafahamu wapo watu wanaishi na risasi katika miili yao bila kuwa na madhara.

Septemba 7 mwaka jana Lissu alipatwa na mkasa wa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa anatokea bungeni Dodoma na kuelekea nyumbani kwake anapoishi.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles