27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Sadc yaja na mafuriko hoteli kubwa

Kufanyika kwa mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc) kumeendelea kutoa fursa kwa Tanzania ambayo ndiyo mwenyeji.

Shughuli za mkutano huo unaotajwa kukutanisha wageni zaidi ya 1,000 kutoka nchi 15 zilianza rasmi Agosti 5 kwa Maonyesho ya Wiki ya Viwanda ya Sadc kisha kufuatiwa na vikao katika ngazi mbalimbali ambavyo vinaendelea.

Wadau mbalimbali, hasa wa sekta binafsi kama vile wasafirishaji, wenye hoteli, taasisi za fedha, watoa huduma za utalii, chakula, burudani na wengine ni miongoni mwa wanufaika.

Kwa upande wa hoteli, nazo zimenufaika, hasa zilizoko katikati ya Jiji la Dar es Salaam, huku nyingine zikiwa ni zile zilizoko Masaki na Mikocheni.

Baadhi ya hoteli zilizofaidika ni Slipway, Double Tree, Amaria (Mikocheni), City Lodge, Doble View, Tropical, Florida, Sea Shells, Southern Sun, Serena, Hyatt, Holday Inn, Amaria (city centre), Tanzania executive suites, Tifany Diamond, Rainbow, Sophia, Peacock, Best Western na Sleep Inn.

Kwa upande wa watoa huduma za usafirishaji, nao wamepata fursa za kukodisha mabasi ambayo yamekuwa yakiwachukua na kuwarudisha wajumbe kutoka mahali walikofikia na sehemu kunakofanyika mkutano huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles