26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Matapeli tisa wa ‘tuma fedha namba hii’ mbaroni

GUSTAPHU HAULE -PWANI

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani limewakamata watuhumiwa tisa wanaodaiwa kujihusisha na matukio ya utapeli wa fedha kwa kutumia simu za mkononi kupitia laini za simu kutoka kampuni mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, alisema watuhumiwa hao walikamatwa Jumanne iliyopita, saa 8 mchana eneo la Zinga wilayani Bagamoyo.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na simu za mkononi 14, laini za kampuni mbalimbali 22, huku wakiwa na orodha ya namba za simu za watu zilizokuwa zimeorodheshwa katika karatasi.

Aliwataja waliokamatwa ni Seleman Athuman (35), Hamisi Iddy (30) anayefanya kazi ya kuuza nyama, Mbwana Magaila (25) kondakta wa daladala, Dipinde Pango (25) mkulima na Adam Nestory (34).

Wengine ni Hamis Kondo (27), Deus Swai (31), Julius Joseph (27) na Mohamed Bruno (33) ambao wanajihusisha na biashara mbalimbali.

Kamanda Nyigesa alisema watuhumiwa hao walikamatwa kutokana na mtego maalumu uliowekwa na askari wake.

“Watuhumiwa hawa ni wale ambao wamekuwa wakitapeli kwa kuwatumia watu ujumbe mbalimbali wa ‘tuma pesa kwenye namba hii’, wengine wanajifanya waganga wa kienyeji, tumewatia nguvuni na tunaendelea na msako huu mpaka kieleweke,” alisema Kamanda Nyigesa.

Alisema wanaendelea kuwahoji na baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.

Alitoa wito kwa wananchi kuwa makini na matapeli wa aina hiyo, huku akitaka watu wafanye shughuli za kujipatia kipato halali kwa kuwa uhalifu hauna faida

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles