25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

SABABU ZA WABANGUAJI KOROSHO KUSHINDWA KUENDELEZA VIWANDA ZATAJWA

Na Florence Sanawa, Mtwara

WAZIRI Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema wabanguaji wa ndani hawapati korosho ghafi za kutosha kuendeleza viwanda vyao kutokana na ugumu uliopo kisheria.

Amesema wabanguaji hao wanahitaji zaidi ya tani 240 kwa mwaka mzima huku msimu uliopita tani 320,000 zikisafirishwa kwenda nje ya nchi.

Akikabidhi eneo kwa mkandarasi la kujenga eneo la wajasiriamali katika eneo la Viwanda vidogo (SIDO), Mkoa wa Mtwara amesema limekuwa ni jambo la kusikitisha kwa kuwa wabanguaji wengi ambao ni wanawake wanakosa malighafi ambazo ni korosho za kubangua kwakutumia mashine hizo.

“Pamoja na kwamba tumeuza tani 320,000 zimeuzwa nje ya nchi ambapo wabanguaji wadogo wanapaswa wapate tani 240 waweze kufanya kazi mwaka mzima.

“Kwa kweli tumeongozwa na sheria kuliko kutumia sheria tunaamani tutaengeneza mazingira mazuri ili wabanguaji wadogo na wakati waweze kupata malighafi,” amesema.

Amesema wawekezaji ni Watanzania wenyewe ambao miaka ijayo watakuwa ndiyo wenye viwanda vya kati na vikubwa ndiyo maana ni rahisi Mtwara kutekeleza dhana ya viwanda kwa kuwa malighafi zipo ambazo ni mashine zilizonunuliwa na serikali kutoka nchini India.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles