29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MFUGAJI AMBURUZA DC CHUNYA MAHAKAMANI

Na PENDO FUNDISHA-MBEYA


MKUU wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa na Ofisa Mifugo wa Halmashauri ya Chunya, Julius Ngwita, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya wakikabiliwa na kesi ya madai ya fidia ya Sh milioni 100.

Madai hayo ya fidia yalifunguliwa na Mwenyekiti wa Wafugaji Wilaya ya Chunya, Shang’ai ole Rapoy, baada ya kudai kwamba DC Rehema alitoa amri akamatwe na kuwekwa mahabusu saa 48 kitendo anachodai ni udhalilishaji.

Kesi hiyo namba 2/2018 ilitajwa mahakamani hapo jana kwa ajili ya kutajwa na ilisikilizwa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Chunya, Desdery Magezi, huku wadaiwa wote wawili wakiwakilishwa na Wakili Faraja Msuya na upande wa mlalamikaji akiwakilishwa na Wakili Faraji Mangula.

Mahakama hiyo iliahirisha kusikiliza shauri hilo baada ya Wakili Msuya kuomba kesi hiyo isogezwe mbele ili aweze kuandaa majibu ya madai kwa pamoja kutokana na mteja wake Ngwita kujibu hoja kupitia wakili mwingine na kuridhia kuondoa majibu ya awali na kuomba hoja zote azijibu yeye.

Julai 27, mwaka jana, Shang’ai akiwa katika Kitongoji cha Izumbi, Kijiji cha Sangambi wilayani Chunya, alikamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani na alikabiliwa na kosa la kuzuia watumishi wa Serikali ambao ni maofisa mifugo kutekeleza majukumu yao wakati wa kupiga chapa mifugo.

Pia Septemba 25, mwaka jana mahakama hiyo ilimuachia huru baada ya kuona hana kesi ya kujibu chini ya kifungu namba 230 cha mwenendo ya mashauri ya jinai sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Baada ya kushinda kesi hiyo, Shang’ai, aliamua kumfungulia DC Rehema na kesi ya udhalilishaji kwa kitendo chake cha kumweka ndani saa 48 ikiwa na Ngwita kutoa taarifa hiyo katika mitandao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles