23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Ryan Giggs kukimbilia Ufaransa

ryan-giggsPARIS, UFARANSA

NYOTA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Ryan Giggs, ameweka wazi kuwa atakimbilia nchini Ufaransa kwa ajili ya kuwa kocha mkuu katika klabu za nchini humo.

Mchezaji huyo ambaye baada ya kustaafu soka alikuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo ya Man United, lakini alikuja kufukuzwa kazi baada ya kocha wa sasa, Jose Mourinho kujiunga na klabu hiyo wakati wa majira ya joto mwaka huu.

Nyota huyo alikuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo kwa misimu miwili akiwa chini ya kocha Louis van Gaal, lakini ujio wa Mourinho ulimfanya awe katika wakati mgumu, ambapo Mourinho aliamua kuja na benchi lake jipya la ufundi.

Giggs alihusishwa kutaka kujiunga na klabu ya Celtic baada ya kuondoka United, lakini hadi sasa hajafanikiwa kupata timu, ila anaamini kuwa baada ya kukosa nchini England basi ana nafasi kubwa ya kuwa kocha nchini Ufaransa.

“Kuna klabu mbalimbali ambazo zimeonesha nia ya kutaka kufanya kazi na mimi, nimekuwa nikiangalia wapi sehemu sahihi kwa kuwa lengo langu ni kutaka kuja kuwa kocha mkubwa kama ilivyo kwa makocha wengine.

“Si kila klabu ambayo inaonesha nia ni lazima nifanye nayo kazi, kikubwa ni kuangalia mipango ya klabu pamoja na manufaa yangu binafsi.

“Nchini England kuna timu nyingi ambazo zilionesha nia ya kutaka kufaya kazi na mimi, lakini hatukufikiana mwisho, hivyo ni wakati sasa wa kugeukia nchini Ufaransa kwa ajili ya kuanza maisha yangu mapya.

“Siangalii nitakuwa katika klabu gani, ila naweza kuwa katika klabu ya Ligi Kuu au Ligi daraja la kwanza, bila ya kujali Ligi lakini ninaamini nitakuwa nchini Ufaransa,” alisema Giggs.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 42, kwa sasa anafanya biashara zake pamoja na kocha wa timu ya taifa ya vijana, Gary Neville. Mbali na kufanya biashara, pia kwa sasa kocha huyo ni mchambuzi wa michezo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles