23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Panga la Omog lafyeka saba Simba

joseph-omogNa ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Mcameroon Joseph Omog, amekabidhi ripoti na mapendekezo yake kwa uongozi wa klabu hiyo, huku akitaka wachezaji saba watemwe katika dirisha dogo la usajili lililoanza Novemba 15, mwaka huu.

Omog kwa sasa yupo nchini Cameroon kwa ajili ya mapumziko, baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku timu hiyo ikiongoza kwa kuwa na pointi 35.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya klabu hiyo, kimewataja wachezaji waliopendekezwa kutemwa na Omog kuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Congo, Mussa Ndusha, kipa Manyika Peter, kiungo mshambuliaji Haji Ugando, beki Abdi Banda, Amee Ally na Emmanuel  Simwanza na kiungo Awadhi Juma.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa, Ndusha na Semwanza wao wana mikataba ya miaka miwili kila mmoja, hivyo huenda wakapelekwa kwa mkopo katika timu nyingine, wakati Banda, Juma, Manyika na Ugando mikataba yao inamalizika mwishoni mwa ligi.

Ally, ambaye anacheza kwa mkopo wa muda mfupi Simba, anatarajiwa kurudishwa katika timu yake ya Azam FC.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, timu hiyo inatarajiwa kuanza kambi Jumatatu, mara baada ya kuwasili kwa Omog.

Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele, alipotafutwa kuhusiana na suala hilo, alisema hawezi kulisemea na badala yake atafutwe Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, ambaye hata hivyo, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles