25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ryan Giggs amalizana na Man United

Ryan Giggs
Ryan Giggs

MANCHESTER, ENGLAND

ALIYEKUWA nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United na baadaye kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo, Ryan Giggs, ameshindwa kuelewana na uongozi wa klabu hiyo hivyo yupo tayari kuondoka.

Giggs aliteuliwa kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo chini ya David Moyes mwaka 2014, kabla ya kuendelea na nafasi hiyo chini ya Louis van Gaal mwaka 2015, lakini ujio wa kocha Jose Mourinho ndani ya klabu hiyo kunamfanya msaidizi huyo kukosa nafasi.

Mourinho amechukua nafasi ya Van Gaal, hivyo kocha huyo amedai kuja na uongozi wake mpya ikiwa na kocha msaidizi ambapo Giggs akaonekana kukosa nafasi.

Hata hivyo, uongozi wa klabu hiyo ulikuwa tayari kumwongezea mkataba Giggs na kumpa nafasi nyingine katika uongozi badala ya kuwa kocha msaidizi wa Mourinho, lakini mchezaji huyo amekataa kwa madai kwamba alikuwa na lengo la kuja kuwa kocha na si kazi nyingine.

Mwakilishi wa Giggs kwa sasa yupo katika klabu hiyo kwa ajili ya kufuatilia madai ya mteja wake kabla ya Mourinho kuanza kazi rasmi ndani ya klabu hiyo.

Giggs mwenye umri wa miaka 42, alianza kujiunga na klabu hiyo huku akiwa na umri mdogo ambapo ilikuwa mwaka 1987 hadi anakuja kustaafu mwaka 2014 kabla ya kuja kuwa kocha msaidizi, hivyo ameitumikia timu hiyo kwa miaka 29.

Amecheza michezo 963 na kufanikiwa kutwaa Ligi ya Mabingwa mara mbili, Ligi Kuu akichukua mara 13, wakati kombe la FA akichukua mara nne.

Kwa sasa Giggs amepata dili la kuwa mchambuzi wa michezo katika kituo cha runinga cha ITV nchini England na tayari ameanza kazi ya uchambuzi katika michuano ya Euro 2016.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles