27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Navy Kenzo: Ku-shoot video Tanzania ni sawa na jipu

Wasanii wa Kundi la muziki wa BOngo Fleva liitwalo Navy Kenzo, Nahreal na Aika walipotembelea ofisi za New Habari (2006) Ltd jana.
Wasanii wa Kundi la muziki wa BOngo Fleva liitwalo Navy Kenzo, Nahreal na Aika walipotembelea ofisi za New Habari (2006) Ltd jana.

NA FESTO POLEA,

WASANII wanaounda kundi la Navy Kenzo, Aika Mareale (Aika) na Emmanuel Mkono (Nahreel) wameweka wazi kwamba ugumu wanaoupata wasanii wanapotaka kuchukua video za nyimbo ama filamu zao umekuwa na urasimu mkubwa, ndiyo maana hukimbilia nchini Afrika Kusini.

Wasanii hao walisema hivi karibuni walijaribu kufanya moja ya wimbo wa msanii wao wanaotaraji kutoa kazi zake hivi karibuni lakini walifukuzwa na hata walipoomba vibali walishindwa kupata kwa wakati.

“Tanzania kuna tatizo kubwa la urasimu, msanii anapoomba vibali kwa ajili ya kushoot video ya wimbo wake, mfano juzi tu tulikuwa tunashoot video ya msanii wetu mmoja pale posta lakini tulifukuzwa tukalazimika kwenda sehemu nyingine za kukodi tukamalizia video yetu. Tanzania ni tatizo hata bendera ya taifa kupata ni tabu hadi tulipokwenda Afrika Kusini ndiyo tukapewa kila tulichotaka hadi bendera ya Tanzania ni ajabu sana ni sawa na jipu,” alieleza Nahreel.

Wasanii hao walitoa dukuduku hilo jana walipotembelea ofisi za Kampuni ya New Habari (2006) Ltd inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa, Dimba na The African pamoja na kutambulisha lebo yao ya The Industry itakayokuwa ikimiliki wasanii watatu, Seline Rosalee na Wildad.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles