24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Royal Tour ya Rais Samia yaanza kuzaa matunda, wawekezaji waanza kumiminika

-Kujenga hoteli zenye hadhi ya nyota tano ‘brand ya Kempinski kwenye Hifadhi za Taifa

Na Mwandishi Maalum.

SHUGHULI za Royal Tour zilizokuwa zikifanywa kwa mara ya kwanza nchini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya Utalii, Biashara na Uwekezaji nchini zimeanza kuzaa matunda kwa wawekezaji kuanza kujitokeza kwa uwekezaji wa hoteli za kisasa ndani ya hifadhi za Taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro.

Hayo yamebainishwa na Serikali kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro mara baada ya mkutano  wake maalum na  Wawekezaji uliofanyika Dar es Salaam mapema leo Septemba22, 2021. Ambapo amekutana na wawekezaji hao kutoka Bara la Ulaya katika nchi ya Bulgaria watakaojenga hotel za Nyota tano ‘brand’  za Kempinski kwenye hifadhi Nne za Taifa nchini.

Waziri Dk. Ndumbaro amesema mpango mkakati wa Rais Samia kupitia kuandaa kipindi cha Royal Tour umeweza kuzaa matunda hayo na wao kwa Wizara wameupokea kwa kwa sasa ni utekelezaji.

”Juhudi kubwa za kimkakati za Royal Tour zilizoendeshwa na rais wetu zimeweza kuzaa matunda ambapo leo tumepokea wawekezaji mahiri kutoka Bara la Ulaya ambao watawekeza kwenye hoteli kwa kujenga hoteli tatu za nyota tano za ‘brand’ ya Kempinski  kwa uwekezaji wa Dola za Kimarekani milioni 72.

”Mkutano wetu huu hii leo umekwenda vizuri sana na Wawekezaji hawa  kwa hiyo unaweza kuipata hoteli ya Kempinski baada ya ujenzi huo kukamilika… Kempinski Serengeti, Kempinski Manyara, Kempinski Tarangire na Kempinski Ngorongoro,” alisem Dk. Ndumbaro.

Waziri Dk. Ndumbaro ameongeza kuwa, ujenzi huo ni mkubwa sana  na unakadiriwa kuanza rasmi mwezi Januari 2022 ambapo amemshukuru  kwa mara nyingine Mhe Rais kwa kuwezesha kuwapigia ‘pass’ na wao kupitia wizara ya Maliasili ni utekelezaji ikiwemo kupokea Wawekezaji katika sekta hiyo ya Utalii.

”Tunaenda kasi tayari hii Royal tour kwangu mimi kama Waziri na Wizara ya Utalii na Maliasili kwa ujumla wake tunaichukulia kama ‘pass’ ya mwisho katika mpira, unapopewa pasi ya mwisho kazi yako wewe ni kufunga tu. Kwa hiyo sisi tumeshafunga ‘Goal’ lingine hilo kuhakikisha kwamba Royal Tour inakuwa na mafanikio zaidi,” alimalizia Waziri Dk. Ndumbaro.

Agosti 28, mwaka huu Rais Samia alianza rasmi kurekodi vipindi vya Royal Tour maeneo mbalimbali ya vuvutio vya utalii na uwekezaji ikiwemo Tanzania Bara na visiwa vya Zanzibar. 

Ambapo katika ziara hiyo ya kuandaa vipindi hivyo kutembelea na kuonesha kwa wageni vivutio mbalimbali vya Utalii, Uwekezaji, Sanaa na Utamaduni vilivyopo nchini na kwa sasa matunda yake yameanza kuonekana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles