28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Jbwai awatamani Diamond, Rayvanny na Harmonize

Toronto, Canada

BARA la Afrika halijawahi kukauka vijana wenye vipaji ambao wanafanya sanaa zao ndani na nje ya bara hili kwa hatua za mafanikio mbalimbali.

Diamond

Miongoni wa vijana hao ni Jbwai, msanii wa kizazi kipya kutoka Cameroon ambaye kwasasa anaishi nchini Canada na leo amefanya mahojiano na MTANZANIA DIGITAL kama ifuatavyo.

SWALI: Kwa ufupi Jbwai ni nani na uliingia vipi kwenye sanaa?

Jbwai: Mimi ni mwanamuziki wa Cameroon, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki niliyezaliwa Septemba 28, 1993. Nilianza kazi yangu ya muziki nilipohamia Toronto Canada, ingawa historia yangu ya muziki ilianza nikiwa mchanga sana.

SWALI : Je unakabiliwa na changamoto gani katika muziki wako ndani na nje ya Canada?

Jbwai: Changamoto yangu kubwa kama msanii wa kiafrika aliyeko Canada ni kwamba sijaunganishwa moja kwa moja na wale mashabiki damudamu ambao ni watu wa Afrika wanaoweza kuhusika kwa urahisi kuupaisha muziki wangu.

SWALI: Je! Ungependa kufanya kazi na wanamuziki gani kutoka Tanzania na Afrika Mashariki?

Jbwai: Msanii wangu anayependwa zaidi nchini Tanzania ambaye napenda sanaa kufanya muziki naye kazi ni Diamond Platnumz ingawa kuna wasanii wengine kama Harmonize na Rayvanny nina mipango ya kufanya wimbo nao kazi hapo mbeleni.

SWALI: Hadi sasa mafanikio gani umepata kupitia muziki wako?

Jbwai: Katika kazi yangu yote ya muziki, nimekuwa na mafanikio mazuri. Nimekuwa na maonyesho mazuri pia nimefanya uhusiano mzuri na watu wengu ambao wamenipa faida kubwa.

SWALI: Kwa nini ulifikiria kukuza muziki wako Afrika?

Jbwai: Afrika ndio mahali ambapo watu wanaupenda zaidi muziki wangu.

SWALI: Una mipango gani kwa mwaka huu haswa nchini Tanzania?

Jbwai: Katika miezi ijayo mpango wangu ni kutembelea Tanzania, kuwa na maonyesho kadhaa na kujiunganisha na mashabiki wangu na kujifunza tamaduni za huko ambazo naamini nitazifurahia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles