27 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

DAWASA Ilala yajidhatiti kukabiliana na upotevu wa maji

Na Nelson Shoo, DAWASA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa kihuduma ILALA imejipanga kukabiliana na upotevu wa Maji kwa kuendesha zoezi maalum la kudhibiti mivujo katika mabomba makubwa yanayopoteza maji kwa wingi ndani ya eneo lake la kihuduma.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la Meneja wa DAWASA Ilala, Mhandisi Honest Makoi amesema lengo la kuendesha zoezi hilo ni kudhibiti kiwango cha Maji kinachopotea na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma.

Amesema kuwa zoezi la udhibiti mivujo ndani ya eneo lake la kihuduma limeanza kutekelezwa katika mtaa wa Uhuru , kata ya Buguruni Malapa.

“Lengo kuu ni kuweza kudhibiti kiasi cha Maji kinachopotea na kusababisha hasara kwa Wananchi na Mamlaka pia,” ameongeza Mhandisi Makoi.

Mhandisi Makoi aliendelea kusema kuwa zoezi hilo linaenda sambamba na kukagua maunganisho ya Majisafi yasiyo halali ili pia kubaini waliojiunganishia huduma ya Maji kiholela na wale waliojenga makazi juu ya miundombinu ya Majisafi.

“Kupitia zoezi hili tumeweza kubaini wananchi waliojenga juu ya miundombinu ya mabomba ya Majisafi, na sisi kama Mamlaka tumewapa muda maalum waweze kubomoa kwani hata sheria inaeleza wazi kuacha umbali wa mita mbili kutoka ilipo miundombinu ya Maji,” ameeleza.

Ally Kaongwa mkazi wa Buguruni malapa ameipongeza DAWASA kwa kuja na mpango huo utakaosaidia kupunguza kiwango cha maji yanayopotea na kuhakikisha yanawafikia wasiokuwa na huduma.

“Kwa upande wetu sisi wakazi wa Buguruni Malapa tunafurahia mpango huu wa DAWASA wa kudhibiti upotevu wa Maji ukizingatia eneo la Ilala ni eneo kongwe ambalo pia lina wakazi wengi hivyo kubadilisha na kukagua miundombinu ya Majisafi itawasaidia wananchi wengine pia kupata huduma ya maji,” alisema Ndugu Ally.

DAWASA inaendelea kupambana na udhibito wa upotevu wa Maji kupitia njia mbalimbali lengo ikiwa ni kufikia upotevu wa Maji wa kiwango cha asilimia 13 ifikapo 2025.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles