29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

GGML yatajwa kinara uwekezaji nchini

Anna Ruhasha, Geita

Mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine Limited kwa kipindi  miaka mitatu iliyopita  kuanzia 2017 hadi 2020 umewekeza kwenye jamii  zaidi Sh bilioni 30, baadhi ya miradi iliyokelezwa ni pamoja na ujenzi wa masoko ya dhahabu mkoni Geita  , kurekebisha baadhi yam iundombinu ya barabara, Afya, Elimu na ujenzi wa eneo la maonesho ya Teknolojia ya madini.

Makamu wa Rais wa Kampuni ya GGML, Saimoni Shayo.

Haya yameelezwa na makamu wa rais wa GGML, Saimon Shayo, Jumatano Septemba 22, mbele ya Waziri  Mkuu Kassimu Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kufungua maonesho ya Nne ya Teknologia na Uwekezaji katika sekta ya Madini yanayofanyika mkoani Geita.

Akizungumza kwaniaba ya sekta  binafsi, Shayo amesema kuwa kampuni ya GGM inayofahari kubwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwekeza katika miradi ya kimkakati na yaki maendeleo.

“Waziri Mkuu miaka mitatu 2017 hadi 2020 , kampuni yetu imewekeza kwenye jamii zaidi ya Sh. milioni 30 , tumejenga soko la Dhahabu Geita mjini, Katoro,na soko la Dhahabu  Katundu. Pia ujenzi wa barabara, katika eneo hilo la maonesho tumetumia million 800 kujenga.

“Niseme pia katika sekta ya elimu tumekamilisha shule mbili shule ya Mganda na Kamena, mh Waziri pia tumechangia ujenzi katika vituo Vinne vya afya Kakubilo Katoro, Kakubilo na Mganza  na Sota Kamene, na kukamilisha zahanati 17 ambazo zinatoa huduma,” amesema Shayo.

Aidha, ameongeza kuwa  kampuni imekamilisha maboma Mia Saba  ya Madara katika Halmashauri ya mji wa Geita na kujenga shule mpya  shule kumi na Tano na kujenga vyumba vya Madarasa 40 ambapo amesema  miundombinu hiyo itasaidia kuinua  uchumi na maendeleo ya mkoa huo.

Pia Shayo ameongeza kuwa kwa kushirikiana  na serikali ya mkoa  kampuni imeanzisha miradi ya mikubwa ya kilimo Cha mpunga na Alizeti  na kuongeza viwanda vya kuongeza  thamani ambapo miradi hiyo itazifikia zaidi ya kaya 300 na kutoa ajira  kwa watu zaidi 1,750 ili wajiongezee vipato na kuondokana na umasikini.

Vilevile mbele ya Waziri Mkuu amesema kampuni ya Mgodi wa Geita jumla y wafanyakazi zaidi 5,000 kati hao asilimia 98 ni watanzania  na mkakati  wa kampuni ni kuwajengea uwezo wafanyabiashara  wa Geita ili kupata fursa zinazotelewa Mgodini.

Waziri wa Madini, Dotto Biteko akitoa  taarifa kwa Waziri Mkuu amesema wizara   imetekeleza maelekezo ya Serikali kuwa makapuni yanayofanyabiashara na migodi mikubwa ni yakitanzania .

“Rais mama yetu Samia Suluhu Hasan alitoa meelekezo mahususi kwa wizara na tasisi zake, la Kwanza alitwambia nendeni mkawasikilize  wachimbaji wadogo, wakati na wakubwa, naomba nikupe  taarifa mh. Waziri Mkuu tangu tumepewe maelekezo hayo mambo makubwa yamefanyika katika wizara  lakini vile kwenye migodi mikubwa inayoendesha uchimbaji hapa nchi,” asema Biteko.

“Uko tulipotoka mh Waziri Mkuu Biashara nyingi ya migodi na watoa huduma  ilikuwa ni makampuni kutoka nje  leo makampuni mengi yanayofanya Biashara na migodi hii ni yahapa nyumbani mfano Mgodi wetu GGM robo ya Kwanza ya mwaka 2021  wametumia fedha Dola za kimarekani Sh bilioni 90.1.

“Kati ya fedha hizo Dola za Kimarekani milioni 80 zote ni watanzania wanao fanyabiashara kwenye huo Mgodi sawa na asilimia 88  kabla ya mwaka 2021 huduma zote  zilizokuwa zikitolewa katika migodi hii 84 peke yake zikitolewa  kutoka kwenyemakampuni ya ndani hatua zote hizi ni zamama yetu Samia,” amesema Biteko.

Akihutubia mamia ya wananchi wakati akufungua Maonesho hayo mkoani Geita Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa licha ya kuipongeza wizara ya Madini pia amesema   serikali ya  awamu ya sita   itachukua hatua  madhubuti ya kulinda na kuendeleza rasilimali hizo kwaajiri ya maendeleo ya watanzania.

Hata hivyo amesema sekta ya Madini  imeendelea kutoa mchango mkubwa   katika uchumi wa taifa pamoja na pato la mtu mmoja moja  hapa nchini  amb apo kwa mwaka 2019  hadi 2021 sekta ya Madini  omeongoza kwa kuingiza fedha za kigeni  Kati ya bidhaa zote ziliouzwa  nje ya nchi  katika sekta imechangia pato asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 3.4 mapato ya 2015.

Kadhalika mh Waziri Mkuu amesema katika sekta ya Madini makusanyo yameongezeka kutoka Sh bilioni 168 ya 2015  hadi kufikia Sh bilion 584.8 kwa mwaka wa fedha 2021, ambapo amesema serikali itaindelea kuimalisha sekta ya Madini kwa kuwezesha kuchangia zaidi ya asilimia 10 ya pato la nchi inapofika mwaka 2025.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles