27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

RONALDO AZINDUA ‘PERFUME’ YAKE

MADRID, HISPANIA

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amefanya uzinduzi wa ‘perfume’ yake ambayo inajulikana kwa jina la CR7 Eau de Toilette.

Mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Ureno, amekuwa akijiingiza kwenye biashara mbalimbali, awali alifanya uzinduzi wa mafuta ya kupaka baada ya kunyoa nywele, mafuta ya ngozi pamoja na mafuta ya kukata arufu ya kwapa.

Uzinduzi huo wa perfume ulifanyika juzi mjini Madrid na kudai kuwa bei yake itakuwa pauni 19 ambazo ni sawa na Sh 55,000 za Kitanzania.

Wakati wa uzinduzi huo, Ronaldo alionesha uwezo wake wa kupiga muziki huku akiwa DJ na kuwafurahisha mashabiki waliojitokeza kwenye uzinduzi huo.

Mchezaji huyo alikuwa anaitumikia timu yake ya Taifa katika michuano ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi. Katika mchezo dhidi ya Islands, Ureno ilifanikiwa kushinda mabao 5-1, nyota huyo alifanikiwa kupachika mabao matatu peke yake.

Mchezo uliofuata dhidi ya Hungary, Ronaldo hakuweza kufunga bao, lakini alitoa pasi ya mwisho katika ushindi wa bao 1-0, bao hilo likifungwa na Andre Silva.

Tayari mchezaji huyo amejiunga na kikosi cha Real Madrid kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu nchini Hispania, hivyo leo hii wanatarajia kushuka dimbani kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu dhidi ya wapinzani wao Levante.

Mchezaji huyo anaamini kikosi chao kipo vizuri kuelekea mchezo huo wa leo huku wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani mbele ya idadi kubwa ya mashabiki wao.

“Kikosi kipo sawa, tumefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo wa leo, hivyo tunaamini tutafanya vizuri kutokana na jinsi tulivyojiandaa,” alisema Ronaldo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles