25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Ronaldinho kutua Ligi ya England

RonaldinhoRIO DE JANEIRO, BRAZIL

NYOTA wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya Barcelona, Ronaldinho, anatarajia kutua nchini England kutokana na ofa anazopata.

Mchezaji huyo ambaye kwa sasa yupo huru tangu alipoondoka katika klabu yake ya Fluminense, amekuwa akitajwa na baadhi ya klabu nchini England ambapo kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kujiunga Februari mwaka huu.

Kaka wa mchezaji huyo ambaye ni wakala wake, Roberto, amesema hadi sasa amepokea ofa zaidi ya mbili kutoka England, hivyo kilichobaki ni kufanya makubaliano.

“Kwa sasa bara la Asia na United States ni sehemu ambazo mchezaji huyo anakubalika kwa hali ya juu, mchezaji huyo anapenda ushindani na bado ana uwezo mkubwa wa kucheza soka na ndio maana anawindwa na baadhi za klabu.

“Hana majeruhi ya kutisha, mwili wake bado upo katika hali nzuri, nadhani kwamba ana uwezo wa kucheza soka kwa zaidi ya miaka mitatu hadi minne,” alisema Roberto.

Hata hivyo, wakala huyo aliongeza kwa kusema kuwa, Ronaldinho kwa sasa haangalii kiasi gani cha fedha ili aweze kujiunga na klabu, ila lengo lake ni kucheza soka.

“Ronaldinho anatamani sana kuendelea kucheza soka, hana mpango wa kuangalia ni kiasi gani cha fedha ambacho anaweza kupewa na kuitumikia timu, kikubwa ni kupata timu ya kuitumikia,” aliongeza.

Ronaldinho aliwahi kuwa mchezaji bora wa dunia wa Ballon d’Or, bado anaendelea kukumbukwa na mashabiki wa soka kutokana na uwezo wake.

Awali mchezaji huyo aliwahi kutaka kujiunga na klabu ya Manchester United kabla ya kujiunga na Barcelona mara baada ya kuondoka klabu ya PSG mwaka 2003.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles