Leicester City kumkosa Vardy wiki mbili

0
899

VardyLONDON, ENGLAND

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Leicester City, Jamie Vardy, atakuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili kutokana na kufanyiwa upasuaji.

Mchezaji huyo wa nchini England, amefanyiwa upasuaji mdogo wa mtoki, hivyo utamfanya apumzike kwa wiki mbili.

Vardy amekuwa na makali msimu huu kutokana na kuongoza katika upachikaji mabao ambapo hadi sasa ana mabao 15 aliyoyafunga kwenye michuano ya Ligi Kuu na kuifanya klabu hiyo kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.

Kocha wa timu ya Leicester City, Claudio Ranieri, amedai kwamba nyota wake huyo alikuwa na moto mwaka 2015, lakini mwaka huu anauanza vibaya.

“Vardy amepata tatizo ambalo litamfanya akae nje kwa muda, lakini ninaamini ataendelea vizuri na kurudi uwanjani kwa ajili ya kuisaidia timu yake.

“Bado nina kikosi kizuri ambacho kinaweza kuendelea kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya,” alisema Ranieri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here