24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Roberto Martinez aitupia lawama FA

Roberto MartinezLONDON, ENGLAND

KOCHA wa Klabu ya Everton, Roberto Martinez, amekitupia lawama Chama cha Soka nchini Uingereza kwa utaratibu wa dirisha la usajili kuwa wazi wakati Ligi Kuu ikiwa inaendelea.

Martinez amesema kuwa hali hiyo itawafanya wachezaji wasifikirie michezo inayokuja na kuwazia juu ya kusajiliwa.

Ligi hiyo imeanza kutimua vumbi mwishoni mwa wiki iliyopita lakini dirisha la usajili linatarajia kufungwa Septemba 1 mwaka huu.

Martinez ameyaeleza hayo baada ya kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Watford kwenye Uwanja wa Goodison Park katika mchezo wa kwanza wa msimu mpya wa Ligi Kuu, huku klabu ya Chelsea ikionesha nia ya kuitaka saini ya beki wake mwenye umri wa miaka 20, John Stones.

“Dirisha likiwa wazi na huku unajiandaa na mchezo muhimu inakuwa sio jambo zuri na sidhani kama FA wako sahihi.

“Ilitakiwa dirisha lifungwe kabla ya kuanza kwa ligi ili kila mchezaji awe anafikiria kuisaidia timu yake baada ya ligi kuanza na sio kufikiria kusajiliwa.

“Ninaamini wachezaji wengi watatoka mchezoni kutokana na kuwa na mawazo ya kusajiliwa na klabu ambazo zinaonesha nia ya kuwasajili, mchezaji kama John Stones na Ross Barkley wanaonekana kuwaniwa na klabu mbalimbali hivyo watashindwa kufanya vizuri kwa sasa,” alisema Martinez.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles