27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Chelsea waikatia rufaa kadi ya Courtois

544 (1)LONDON, ENGLAND

KLABU ya Chelsea imekata rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyooneshwa mlinda mlango wao,Thibaut Courtois, katika mchezo uliopigwa Jumamosi dhidi ya Swansea ambao timu hizo zilitoka sare ya 2-2, kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kufungua Ligi Kuu England kwa klabu hizo, huku Chelsea wakianza vibaya kwa mlinda mlango wake namba moja kuoneshwa kadi nyekundu na nafasi yake kuchukuliwa naAsmir Begovic.

Mlinda mlango huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23, alitolewa nje dakika ya 52 baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa Swansea City, Bafetimbi Gomis,katika eneo la hatari.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kocha Jose Mourinho, alishindwa kuongelea uamuzi huo ambao ulitolewa na mwamuzi Michael Oliver dhidi ya mlinda mlango wake.

Kutokana na kadi hiyo, Chelsea imeamua kukata rufaa ambayo inatarajiwa kusikilizwa na Chama cha Soka nchini Uingereza (FA) na kama wakikataliwa basi mchezaji huyo ataukosa mchezo dhidi ya Manchester City siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Etihad.

“Penalti ilikuwa ya wazi, lakini mwamuzi hakuwa sahihi kutoa kadi nyekundu kwa kosa hilo, hayo yalikuwa maamuzi magumu kwa Michael Oliver ambaye ni mwamuzi chipukizi,” alisema Mourinho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles