Amir Khan kupigana na Manny Pacquiao

0
725

Pacquiao na KhanLAS VEGAS, MAREKANI

BAADA ya bondia, Floyd Mayweather, kuachana na pambano la Amir Khan na kumchagua Andre Berto, Khan ameamua kuomba pambano dhidi ya Manny Pacquiao.

Mayweather anatarajia kupigana pambano lake la mwisho Septemba 12 mwaka huu dhidi ya Berto, awali Khan alimuomba Mayweather kupambana katika pambano hilo lakini Mayweather aliamua kumchagua Berto.

Kutokana na hali hiyo, Khan anatarajia kupambana na Pacquiao mwanzoni mwa mwaka 2016.

Mwandaaji wa pambano hilo ambaye ni wakala wa Pacquiao, Bob Arum, amesema kuwa pambano hilo litafanyika mapema mwakani huku maandalizi yakianza kufanyika.

“Khan ni kijana mdogo ambaye anaonekana kuwa na uwezo mzuri, ninaamini pambano litakuwa zuri kutokana na ubora wa mabondia wote.

“Lengo kubwa pambano hilo lifanyike Las Vegas nchini Marekani, lakini kuna uwezekano mkubwa wa kufanyika Mashariki ya Kati au Dubai na kama ikishindikana huko kote basi pambano hilo litafanyika Vegas nchini Marekani,” alisema Arum.

Arum aliongeza kuwa, Pacquiao kwa sasa anaendelea vizuri bega lake ambalo aliumia katika maandalizi ya pambano dhidi ya Mayweather, hivyo kuanzia mwakani atakuwa tayari kwa ajili ya kupigana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here