Minaj atembelea hospitali ya watoto Philadelphia

0
637

nicki-minajPHILADELPHIA, Marekani

NYOTA wa muziki wa Hip Hop kwa wanawake nchini Marekani, Nick Minaj, juzi aliwatembelea watoto katika hospitali ya Philadelphia nchini Marekani.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Minaj aliandika kuwa anajisikia furaha kutembelea hospitali hiyo na kufanya mazungumzo na watoto hao.

“Ninaamini watoto wamepata faraja kubwa kuniona na mimi nimejisikia kuwa na furaha kubwa kwa kuwa nimewaombea kwa Mungu ili wapone haraka.

“Nilikuwa na furaha kubwa kuwaona watoto wakiwa na furaha baada ya kuniona, hii inaweza kuwapa afya njema kutokana na aina ya magonjwa yao,” alisema Minaj.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here