22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wenger adai kufungwa na West Ham sawa na ajali

wengerLONDON, ENGLAND

BAADA ya Arsenal kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya West Ham mwishoni mwa wiki iliyopita, kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger, amesema kuwa kufungwa kwa mchezo huo ni sawa na ajali.

Wenger amesema kuwa timu yake ilipata ajali kufungwa na West Ham, hivyo inajipanga ili kuweza kufanya vizuri michezo ijayo.

”Tupo katika maumivu kutokana na kidonda tulichopata dhidi ya West Ham,ninaamini kila kitu kitakuwa sawa kwa michezo ijayo,” alisema Wenger.

Arsenal licha ya kumiliki mpira kwa asilimia 62 na kupiga mikwaju 22 katika lango la mpinzani,lakini ilishindwa kufanya vizuri katika uwanja wa nyumbani wa Emirates na kuambulia kichapo hicho cha mabao 2-0.

“Nilijua huenda ikawa mechi ngumu,lakini iwapo unajua huwezi kushinda mechi basi hakikisha kuwa huipotezi huku ukiweka ulinzi wa hali ya juu.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles